ONA SASA
Leo jioni wakati natoka katika shughuli zangu nilipita maeneo ya Mwenge pale stand ya mabasi nimekuta kweupe wale vijana wanao uza nguo kwa kupanga chini na kuzishika sikuwaona ...nikauliza nikaambiwa wamefukuzwa kwa ajili Oboma Anakuja...Mmhhh Kazi kweli kweli.
Wakati bado nashangaa shangaa Mara likaja gari la Polisi na Wale mgambo wa jiji...Mara nikaona watu wanakimbia huku na kule.
Kushangaa kumbe wale wamachinga bado wapo ila wanauza kwa kujificha ficha kwenye vichochoro vya maduka..Sasa Kimbembe kikaanza wale wanamgambo wakawafuata huko huko na kuanza kuwapiga na kuwavunjia meza na viti vyao.
Kwa kweli iliniuma sana kuona watanzania wenzetu wakifanyiwa hivyo ....Bado sijapata jibu ...siko zote mbona hawakufukuzwa ?? Huu Ugeni ndio imekuwa Nogwaaaaa.
Na uhakika kuna ambao wanalisha na kutunza familia kwa kazi hizi za umachinga sasa watakula wapi kama hali ndio hiyo. ?
No comments:
Post a Comment