WAKATI wafanyabiasha ya ukahaba jijini Dar es Salaam wakijipanga kutekeleza kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe, yakuwataka watanzania kuchangamkia biashara zao na kutokubali wageni warudi na dola makwao, Jeshi la polisi limejipanga kuwadhibiti.
Wakizungumza na habarimpya.com makahaba hao waliokuwa wamejipanga kujipatia pesa za kigeni kutoka kwa baadhi ya wageni ambao wangewahitaji, walisema Askari Polisi wamejipanga kuvuruga biashara zao.
Hatua ya Jeshi la Polisi kuendelea kuwasaka makahaba hao imezidi kuvuruga mipango yao ya kupata dola chap chap, oparesheni ina yozidi kufanyika hasa maeneo ya Kinondoni, pengine ikabunguza dola chap chap kama alivyo agiza Membe.
“Kwa kweli mpaka sasa hatujaelewa itakuwa vipi kwani ni kitu cha ajabu sana na imekuwa tofauti na matarajio tuliyokuwa tumejiwekea,mwanzoni tuliifurahia sana kauli ya waziri Membe iliyosema,watanzania tuchangamkie biashara zetu, tusizubae wageni warudi na dola zao kwao sasa naona imekuwa kinyume kwani ulinzi uliopo ni balaa” alisema mmoja wa makahaba aliyejitambulisha kwa jina la Zamda aliyesafiri kutoka Dodoma kuja jijini Dar es Salaam.
Mbali na Makahaba, wamachinga pia wameonekana kukosa maeneo ya kufanyia biashara zao katika maeneo mabalimbali ya jiji, baada ya Polisi kuongoza oparesheni hiyo inayoendelea sehemu mbalimbali za jiji hilo.
Akizungumza na Habarimpya.com Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Camillus Wambura alisema, “Tumeamua kuimarisha ulinzi wa Jiji na kuliweka safi jiji letu, sio kwa ajili ya ujio wa Rais Obama tu, bali hii oparesheni mpya itakayo endelea kufanyika ndani ya jiji hili hata wageni hawa pindi watakapo ondoka, tumeamua kuifanya Kinondoni kuwa mpya kwa kuzuia mambo yote yanayotendeka kinyume cha sheria”.
No comments:
Post a Comment