Tuesday, May 20, 2014

BABA WA TAIFA AIKANYA TANZANIA KWAKUMTOKEA MKEWE NDOTONI


MKE wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria, amesikitishwa na jinsi baadhi ya watu wanavyomkosoa mwasisi huyo kwa kuwa enzi za uhai wake alifanya kazi kwa bidii katika kulitumikia taifa kiasi cha wakati mwingine kuisahau familia kwa muda.

Akiongea na waandishi nyumbani kwake Msasani, jana, Mama Maria alisema kwa uchungu kuwa mumewe ambaye alifariki miaka 15 iliyopita, amemtokea ndotoni na kumtaka akalitahadharishe taifa na mwenendo wake.

“Kitendo cha nchi kukumbwa na mashetani wanaovuruga amani na kutukana waasisi kimemfanya Mwalimu Nyerere kunitokea na kunitaka kuliambia taifa kusali na kuomba sana kwani nchi inaelekea katika vita” Alisema jana huku akionesha hisia kali.

Pia, alisema mambo yanayoendelea nchini kwa sasa ni matokeo ya tamaa na kupungua kwa upendo miongoni mwa jamii jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi.

Mama Maria alisema ukosoaji wa viongozi waasisi ni tatizo la dunia nzima ambalo limekuwa jinamizi kama ilivyotokea kwenye nchini mbalimbali ikiwemo Misri na Libya, hivyo ili Tanzania iweze kuepukana nalo ni wajibu wa kila mtu kuombea taifa kwa kufikiria tulikotoka na tulipo.

Alisema ni wazi kuwa Mwalimu Nyerere alifanya kazi kwa bidii hata kuisahau familia muda mwingine, kwa sababu aliwapenda Watanzania pasipo ubaguzi wowote na kama alikosea mahali ilitokea kwa kuwa na yeye ni binadamu.

No comments:

Post a Comment